:: Home :: About Us :: NGO Profiles :: NGO Board :: Site Map :: Feedback :: Contact Us   :: NGOs MIS  
      KEY AREAS
Youth Empowerment  
Agriculture  
Capacity Building  
Economic Empowerment  
Education  
Environment  
Good Governance  
Health  
HIV/AIDS  
ICT  
Legal Rights  
Multi Sectors  
People with desability  
Poverty Alleviation  
Service Sector  
 
  USEFUL LINKS
a
Fanya Malipo ya Ada za NGOs
a
President's Official Website
a
National Council of Ngo's
Ministry of Community Development,Gender and Children
Tanzania National Website
Community Development Insititutes
Tanzania Development Gateway
United Republic of Tanzania, Wananchi Portal
  More Links >>

 

 
  INTRODUCTION  
 
BODI INAUNDWA NA NANI?
Bodi ya Taifa ya Uratibu wa NGOs ni chombo cha juu cha usimamizi wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.Chombo hiki kimeundwa kwa mujibu wa Sheriaya NGOs Na.24 ya mwaka 2002 Kifungu cha 6(1).Sheria hii imeweka utaratibu wa kuanzisha vyombo vikuu viwili vya kitaifa, yaani Bodi ya Taifa ya Uratibu wa NGOs (National NGOs Coordination Board) na Baraza la Taifa la NGOs (National Council for Non Governmental Organizations)
Bodi ya  Taifa ya Uratibu wa NGOs ilianza kazi yake rasmi tarehe 20 Aprili 2004 kwa uzinduzi uliofanywa na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Kuondoa Umasikini na Uratibu wa NGOs, Mh. Maokola Majogo.Aidha, katika mabadiliko ya Wizara yaliyofanyika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne, jukumu la kuratibu NGOs limewekwa chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kuanzia mwezi Februari 2006.

 

DIRA YA BODI

Kuona Mashirika Yasiyo ya Kiserikali imara na kuhakikisha kuwepo na mazingira bora mazuri yatakayowezesha NGOs kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, kuongeza ushirikiano na Serikali pamoja na wadau wengine na hivyo kuchangia kikamilifu katika kupunguza umaskini na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

 

UTUME WA BODI (MISSION)

Utume wa Bodi ni kuratibu, kusimamia usajili wa NGOs na kuwezesha uendeshaji wa shughuli za NGOs nchini kwa mujibu wa Sheria ya NGOs kwa kushirikisha wadau wote.

 

UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI

Bodi ina jumla ya  wajumbe kumi (10) kati ya hayo Mwenyekiti huchaguliwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano baada ya kupokea mapendekezo kutoka kwa Waziri anayesimamia mashirika yasiyo ya kiserikali.
Wajumbe wanne (4) huteuliwa na Waziri kwa mapendekezo kutoka Baraza la Taifa la NGOs, wajumbe hawa huwakilisha sekta ya NGOs. Aidha wajumbe wengine watano ( 5) huchaguliwa na Waziri kwa kuzingatia uzoefu wao katika kulitumikia Taifa, hawa huwakilisha upande wa serikali.  Kati ya wjaumbe hawa watano (5) Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO's Coordination Department) huwa ndiye katibu wa Bodi  kwa wadhifa wake.
MAJUKUMU YA BODI
 1. Kuidhinisha na kuratibu usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali
 2. kuwezesha utekelezaji wa sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ( NGOs)
 3. Kuwezesha uratibu wa shughuli za mashirika yasiyo ya Kiserikali ( NGOs)
 4. Kuidhinisha maombi ya usajili au ya vyeti vya ukubalifu
 5. Kutoa maelezo juu yai ya kusimamishwa au kufutiwa usajili shirika lolote lisilo la kiserikali
 6. Tathmini ya taarifa mwaka  za utekelezaji wa shughuli za mashirika yasiyo ya Kiserikali ( NGOs)
 7. Kuishauri serikali kuhusiana na shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali
 8. Kupitia rejista ya mashirika yasiyo ya kiserikali.
 9. kutoa miongozo ya kisera kwa mashirka yasiyo ya kiserkali kwa ajili ya kuoanisha shughuli za mashiruika hayo na mpango wa Taifa wa maendeleo.
 10. Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa za kawaida za baraza, na kutoa ushauri wa mkakati endelevu utakaowezesha usimamizi thabiti wa shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali.
 11. kuwezesha kuwepo kwa miundombinu na mitandao ya  upashanaji habari kati ya mashirika yasiyo ya kiserikali na Serikali.
 12. kuchunguza na kuhoji jambo lolote ili kuhakikisha Shirika Lisilo la Kiserikali linazingatia katiba yake na kwa mujibu wa sheria.
 13. kufanya shughuli yoyote kama itakavyoagizwa na waziri muhisika.
VIKAO VYA BODI NA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU
Kisheria Bodi ya Taifa ya Uratibu wa NGOs inatakiwa kukutana mara moja kila baada ya miezi mitatu.Hata hivyo inaweza kufanya kikao cha dharura wakati wowote ikibidi. Ili kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, Bodi imekasimu baadhi ya majukumu yake kwa Sekretarieti yaani Idara ya Uratibu wa Shughuli za NGOs. Utekelezaji wa majukumu haya unasimamiwa na Mkurugenzi wa NGOs ambaye ndiye Katibu wa Bodi kisheria. Hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 2 (b) cha Sheria ya NGOs Na.24 ya mwaka 2002

 

WAJUMBE WA BODI ( 2019 - )

 

 
  :: Home :: About Us :: NGO Profiles :: Site Map :: Feedback :: Contact Us